24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Migogoro ya wakulima na wafugaji Kiteto yapata suluhisho

Mohamed Hamad, Kiteto

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Mhandisi Tumain Magesa amesema uanzishwaji wa nyanda za malisho wilayani humo ni kutaka kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji na ndio maana zinakuwa chini ya kijiji husika.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Dosidosi Januari 10 mwaka huu, alipokuwa akiwatolea ufafanuzi juu ya uanzishwaji huyo  DC Magesa alisema kuna bàadhi ya wananchi wanapotosha umma juu nyanda hizo.

“Kimsingi kinachofanyika ni Wizara ya Mifugo kutaka kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuja na mkakati uliopo kwenye Ilani ya CCM na kuutekeleza kwa kutengeneza nyanda hizo, ” alisema.

Alisema nyanda za malisho zinaanzia kijijini kwa wananchi wenyewe kujadiliana na kufikia muafaka, uelewa wa wananchi umekuwa ukisumbuliwa na baadhi ya watu  wakisema kuwa hifadhi zimeongezeka sana wengine nyanda za malisho na kuwataka wawe makini.

Aidha Magesa alizitaja  nyanda hizo kuwa ni Olengapa na  Alole zilizopo tarafa ya Kijungu na Napalay iliyopo Kata ya Partimbo ambapo alidai kuwa zipo katika hatua za ukamilishwaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles