‘Migogoro imesababisha kushuka kwa biashara Tanzania, Kenya’

0
797

Derick Milton SimiyuBalozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu, amesema migogoro ya kibiashara kati ya Tanzania na Kenya imesababisha kushuka kwa kiasi kikubwa ufanyaji wa biashara kati ya nchi hizo.

Balozi Kazungu amesema hayo leo Ijumaa Oktoba 5, wakati akizungumza na wafanyabishara katika kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery, kilichpo wilayani Bariadi, mkoani Simiyu akiwa katika ziara ya siku moja mkoani hapa.

“Miaka mitano nyuma, biashara kutoka Kenya kuja Tanzania ilikuwa na thamani ya Sh bilioni 46 kwa fedha ya kenya, huku Tanzania kwenda Kenya ilikuwa Sh bilioni 34 hadi 35 kwa fedha ya Kitanzania.

“Lakini hivi sasa biashara kwa nchi hizo, imepungua kutoka bilioni 46 kwa fedha ya Kenya biashara kutoka Kenya kuja Tanzania na kufikia Sh bilioni 28 na Tanzania kwenda Kenya kwa fedha ya Tanzania ambayo imeshuka hadi kufikia Sh bilioni 20 kutoka bilioni 35,” amesema.

Aidha, Balozi Kazungu amesema kuwa uamuzi wa Rais John Magufuli kuazisha mradi mkubwa wa umeme Stiegler’s George ni sahihi na nchi ya Kenya inaunga mkono na kuongeza kuwa mradi huo utasaidia kukuza uchumi wa Tanzania na Kenya.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Kazungu ameahidi kuleta wawekezaji kutoka Kenya kuja mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuwekeza mkoani humo hasa kujenga kiwanda cha pamba, kutokana na mkoa huo kuzalisha zaidi ya asilimia 50 ya zao hilo nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here