Imechapishwa: Thu, Aug 10th, 2017

MIFUGO KUPIGWA CHAPA

 

WAFUGAJI mkoani Geita  wamehimizwa kujitokeza  kupiga chapa mifugo yao kwa kuwa hatua hiyo inasaidia kudhibiti wizi wa mifugo na kuwafanya kuitambulika haraka, anaripoti Harrieth Mandari.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi alisema pamoja na idadi kubwa ya wafugaji kujitokeza, bado viongozi na watendaji wanapaswa kuendelea kuwahimiza wafugaji waliosalia  kujitokeza na kupiga chapa ng’ombe wao.

Alisema   upigaji chapa ni agizo la Waziri Mkuu aliyetaka    ng’ombe wote nchini wapigwe chapa   kuondokana na tatizo la wimbi la wizi wa mifugo na pia kusaidia kujua takwimu kamili za ng’ombe nchini.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

MIFUGO KUPIGWA CHAPA