31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mhasibu Wizara ya Afya ashikiliwa kwa ubadhirifu wa fedha za chanjo

Upendo Mosha, Moshi

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), mkoani Kilimanjaro inamshikilia Mhasibu  wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa tuhuma za kufanya ubadhirifu wa  zaidi ya Sh milioni 34 katika fedha za chanjo ya Rubella.

Akizungumza na waandishi wa habari leo  Juni 11, Mjini Moshi, Kamanda wa TAKUKURU, mkoani hapa, Holle Makungu, amesema  taasisi hiyo inamshikilia Mhasibu huyo kutokana na kufanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 22 na 28 vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Amesema mhasibu huyo ambaye anajulikana kwa jina la Yahya Athuman, alimdanganya mwajiri wake na kufanya ubadhirifu wa fedha za umma zaidi ya Sh milioni 34.2.

Aidha amesema Uchunguzi wa TAKUKURU unaonyesha kuwa mwaka 2014 wizara iliendesha zoezi la chanjo ya Rubella katika halmashauri mbalimbali ikiwemo halmashauri ya Moshi Vijijini na kwamba  wahasibu kutoka wizara hiyo walipewa jukumu la kusimamia fedha hizo na kufanya ubadhirifu huo.

“Sh milioni 491.8 ziliwekwa kwenye akaunti na zilikuwa na maelekezo na Yahya alikabidhiwa ili asimamie matumizi katika Halmashauri za Manispaa ya Moshi, Moshi vijijini, Siha, Hai, Rombo, Mwanga na Same “amesema.

Makungu amesema katika mgawanyo wa fedha hizo halmashauri ya Moshi Vijijini ilikuwa ni Sh milioni 99 na uchunguzi umebaini kuwa kati ya fedha hizo Yahya aliandaa na kuwasilisha nyaraka za udanganyifu kwa mwajiri wake  ambazo zilisababisha ubadhirifu wa fedha hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles