Mhadhiri UDSM achambua tatizo la wakimbizi

0
788

Leonard Mang’oha, Dar es Salaam

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Khoti Kamanga, amesema tatizo la wakimbizi haliwezi kukomeshwa katika taifa hata kama serikali ya taifa husika itachukua hatua kali kupambana na tatizo hilo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Oktoba 5, jijini Dar es Salaam na katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya wakimbizi.

Profesa Kamanga amesema tatizo hilo haliwezi kumalizika kwa sababu si jipya na kwamba limekuwapo muda mrefu na limeoneshwa hata katika vitabu vitakatifu.

“Si tatizo jipya ni la muda mrefu hata katika misahafu na biblia. Kwa hiyo hata serikali zikichukua hatua gani halitatoweka.

“Kwa sasa kumekuwa na tatizo kubwa la kuwapokea wakimbizi katika mataifa mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania kutokana na baadhi ya mataifa yemekuwa yakiweka vipingamizi vingi vya kuwazuia wakimbizi kupata hifadhi katika mataifa hayo,” amesema.

Aidha, amesema pamoja na mataifa mbalimbali kuwapokea na kuwapa hifadhi wakimbizi wamekuwa chanzo cha matatizo ikiwapo vurugu na na ujambazi hasa kwa wakimbizi wanaotoka katika mataifa yenye vita.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here