24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mgonjwa wa Ukimwi athibitishwa kupona

LONDON, UINGEREZA

Mwanaume mmoja kutoka London, Uingereza, amethithitishwa kuwa ndiye mtu wa pili kupona virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi, wamesema madaktari.

Adam Castillejo bado hajapatikana na virusi baada ya kukaa siku 30 bila kumeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV zinazofahamika kama anti-retroviral.

Hata hivyo, madaktari walieleza kuwa hakupona kutokana na dawa za HIV, bali kwa tiba ya uboreshaji wa seli alizopewa kwa ajili ya matibabu ya saratani ambayo alikua nayo, limeripoti jarida la kitabibu la The Lancet linaloandika juu ya HIV.

Watoaji wa seli hizo wana geni zisizo za kawaida ambazo walimpa Castillejo, ambazo zilikuwa kwa ajili ya ulinzi dhidi ya HIV.

Mwaka 2011, Timothy Brown, “mgonjwa Berlin ” alikua ni mtu wa kwanza kuripotiwa kuwa amepona HIV, miaka mitatu na nusu iliyopita baada ya kupata tiba sawa na hiyo.

Tiba ni ipi?                                        

Upandikizaji wa seli zinazoboresha seli nyingine au “Stem-cell transplants” unaonekana kuzuia virusi hivyo kuendelea kuwa na uwezo wa kuzaana mwilini ndani ya mwili kwa kuchukua nafasi ya mfumo wenyewe wa seli za kinga za mwili na kutumia seli za mtoaji ambazo zinazuia maambukizi ya HIV.

Adam Castillejo (40)- “Mgonjwa wa London” ambaye aliamua kutangaza utambulisho wake mwenyewe, hana virusi vya HIV katika damu yake, maji maji ya mwili au nyama za mwili wake, madaktari wake wamesema.

Ni mwaka mmoja sasa baada ya kutangazwa kwa mara ya kwanza kuwa hana virusi vya HIV.

Mtafiti wa Lead, Profesa Ravindra Kumar Gupta, kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge, aliiambia BBC kuwa hii inaonesha kuwa tiba ya HIV karibia inawezekana na sasa wamekuwa na miaka wawili na nusu ya kutotumia madawa ya kupunguza makali ya HIV.

“Matokeo ya uchunguzi wetu yanaonesha kuwa mafanikio ya matumizi ya upandikizaji wa seli mbadala kutoka kwa mtu mwingine kama tiba ya HIV, kwa mara ya kwanza yaliripotiwa miaka tisa iliyopita katika mgonjwa wa Berlin na yanaweza kunakiliwa,” alisema

Lakini haitakua tiba kwa mamilioni ya watu kote duniani wanaoishi na virusi vya HIV.

Tiba hii awali ilitumiwa kutibu saratani ya wagonjwa, sio virusi vya HIV

Na dawa za hivi karibuni za HIV bado zinafanya kazi, ikimaanisha kuwa watu wenye virusi vya HIV wanaweza kuishi maisha marefu na ya afya.

Profesa Gupta alisema: “Ni muhimu kufahamu kuwa tiba hii inayoponya ni ya hatari ya hali ya juu na hutumiwa tu kama tiba ya mwisho kwa wagonjwa wenye HIV ambao wanakabiliwa na hatari ya ukosefu wa damu kutokana na uvimbe wa saratani.

“Kwa hiyo, hii sio tiba ambayo inaweza kutolewa kwa wagonjwa wengi wenye kupata mafanikio ya tiba ya madawa ya kupunguza makali ya HIV.”

Alisema lakini inaweza kutoa matumaini ya kupata tiba, katika siku zijazo, kwa upandikizaji wa jeni.

Profesa Gupta alisema CCR5 hutumiwa kwa kawaida kwa watu wenye HIV-1, aina ya virusi vya HIV inayopatikana kwa wingi kote duniani, inayoingia katika seli.

Alisema lakini kila idadi ndogo sana ya watu ambao huwa wana kinga ya mwili ya HIV wana nakili mbili za CCR5 zinazoweza kubadilika umbo lake.

“Hii inamaana kuwa virusi haviwezi kupenya katika seli katika miili ambayo kwa kawaida huweza kuambukizwa,” alisema.

Watafiti wanasema inawezekana kutumia jeni kulenga wapokeaji wa katika watu wenye HIV.

Je ni tiba ya kudumu?

Vipimo vinaonyesha kuwa asilimia 99 ya kinga ya seli za Castillejo ziliondolewa na kuwekwa zile za mtoaji, lakini bado ana virusi vichache katika mwili wake, kama ilivyo kwa Brown.

Na inawezekana kusema kwa uhakika virusi vya HIV havitarudi katika mwili wake.

Castillejo aliliambia gazeti la New York Times: “Hii ni fursa niliyo nayo, na kushukuru sana . Ninataka kuwa balozi wa matumaini. Sitaki watu wafikirie, oh  ulichaguliwa, hapana, ilitokea tu. Nilikua mahala panapofaa, labda kwa wakati, ilipotokea,” alisema.

Profesa Sharon Lewin, kutoka Chuo kikuu cha Melbourne, Australia, alisema: “Kutokana na idadi kubwa ya sampuli za seli zilizokusanywa hapa na ukosefu wa virusi, je mgonjwa wa London amepona kiukweli? “Data nyingine zilizotolewa katika ufuatiliaji wa kisa zinatia moyo lakini kwa bahati mbaya, mwishowe, tutajua ukweli baada ya muda .”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles