MGOMBEA UVCCM AMTUHUMU MBUNGE KUTOA RUSHWA KUMWANGUSHA

1
5

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}

Aliyekuwa mgombea katika uchaguzi wa Umoja ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Simon John, amemtuhumu Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, Richard Mbogo (CCM), kuwahonga Sh 20,000 wajumbe walioshiriki katika uchaguzi huo uliofanyika hivi karibuni na kumnyima yeye ushindi.

Aidha, mgombea huyo amegoma kusaini fomu za matokeo ya uchaguzi akidai uligubikwa na rushwa  kwa wajumbe kuhongwa Sh 20,000 ambapo yeye aliambulia kura 98 huku mpinzani wake Mwavi Martin, akiibuka kidedea kwa kupata kura 160 na kutangazwa mshindi.

“Baadhi ya viongozi wasio wadilifu na wanaoendekeza rushwa ili kununua uongozi  walidiriki kutoa rushwa ya Sh 20,000 kwa kila  mjumbe aliyekuwa na sifa ya kupiga kura ili wampigie kura mgombea waliyekuwa wakimtaka  wao,” amesema.

Kwa upande wake Mbogo amekanusha vikali madai hayo akisisitiza kuwa kama kuna mtu au mgombea  mwenye ushahidi aende mahakamani huku msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Diwani Kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda, Haidary Sumry akisema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki.

Kutokana hali hiyo, mgombea huyo amesema tayari ameshawasilisha tuhuma hizo za rushwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Jeshi la Polisi na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Katavi ambapo pia amekata rufaa kupinga matokeo hayo.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here