MGOMBEA URAIS BRAZIL ACHOMWA KISU

0
576

Brazil


Mgombea urais nchini Brazili, Jair Bolsonaro, amechomwa kisu wakati akiwa katika harakati za kampeni zake kuelekea uchaguzi nchini humo.

Bolsonaro, alichomwa kisu alipokuwa katika mkutano uliokuwa na mkusanyiko wa watu wengi katika eneo la kusini mashariki mwa Brazili.

Mwanasiasa huyo ambaye amekua gumzo kwa maoni yake juu ya ubaguzi wa rangi, ameongoza kwa kupata kura nyingi katika kura za maoni zilizofanyika hivi karibuni zinazoonyesha ubashiri wa kufanya vizuri katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Baada ya shambulio hilo, mtoto wa Bolsonaro, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba.

”Kwa bahati mbaya amekua na hali mbaya kuliko tulivyodhani, amepoteza damu nyingi amefika hospitali na damu 10/3, lakini sasa anaendelea vizuri tafadhali tumuombee.”

Wauguzi wa hospitali hiyo walisema Bolsonaro, amepata jeraha kubwa kwenye utumbo lakini sasa anaendelea vizuri.

Hata hivyo polisi wa eneo hilo wamesema kuwa tayari wamemkamata muhusika wa tukio hilo ambaye ni Adelio Obispo de Oliveira .

watu mbalimbali wamemlaani vikali muhusika huyo kwa kitendo alichokifanya.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here