MGOMBEA CHADEMA AENGULIWA KWA KUSHINDWA KUSOMA NA KUANDIKA

0
503

Na Eliya Mbonea, Arusha

Mgombea udiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Kamwanga, Sakimba Nakutamba ameenguliwa kugombea nafasi hiyo kutokana na kutojua kusoma na kuandika.

Kutokana na hali hiyo, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elias Laizer amepita bila kupingwa.

Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Longido, Juma Mhina, amethibitisha uhalali wa pingamizi lililowekwa na mgombea CCM kwani mgombea huyo alishindwa kujaza fomu za kugombea na kuzirejesha bila kujaza kutokana na kushindwa kusoma na kuandika.

“Mgombea huyo, alishindwa kujaza fomu namba 10, hata alipopelekewa barua ya pingamizi hakuweza kuijibu hadi muda aliotakiwa kuresha majibu ofisini ulipomalizika,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here