27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MGOMBEA CHADEMA ADAI ATASHINDA ‘ASUBUHI TU’ SIHA

Na Mwandishi wetu –


Mgombea ubunge wa Jimbo la Siha, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Elvis Mosi, amesema atashinda ubunge wa jimbo hilo mapema asubuhi kutokana na mgombea aliyepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Godwin Mollel, kutokuwa na nguvu ya kushinda kwani amekosa sifa za kuwa kiongozi kwa madai kuwa ni mtu mwenye tamaa na asiyekuwa na msimamo.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumamosi, mgombea huyo amesema chama chake kimemuamini na kumpitisha baada ya kumpima na kuona anao uwezo wa kukabiliana na Dk. Mollel na kwamba ushindi wake utapatikana asubuhi.

“Mgombea wa CCM hawezi kamwe kushindana na mimi yaani ni ardhi na mbingu na sifa ya kumshinda tunayo, kwanza ni mtu aliye na tamaa na asiyekuwa na msimamo wananchi hawawezi kumchagua mtu wa namna hiyo kwani walimuamini lakini amewasaliti,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles