33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mgeja atoa neno ununuzi wa mazao

Mwandishi Wetu -Kahama

WAKULIMA  wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuanza kuwajali wakulima wa Mazao mbalimbali kwa kuchukua hatua ya kuwakomboa kwa kutoa maelekezo ya kulielekeza shirika la Taifa la kuhifadhi chakula (NFRA) kununua mazao myote katika  msimu huu.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nyanhembe Agricultural Farm,  Khamis Mgeja ambayo  inayojishughulisha na shughuli za Kilimo na ufugaji alipotembelewa na jopo la waandishi wa habari kwenye shamba lake la mpunga lililopo Kijiji cha Nyanhembe wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Alisema wakulima wamemsikia na kumuona hivi karibuni Waziri wa Kilimo,  Japhet Hasunga akiwa mkoani Manyara akitoa maelekezo kwa kwa Shirika la Taifa la Kuhifadhi Chakula (NFRA),  ikiwemo na zao la mpunga na kuacha kasumba iliyozoeleka misimu iliyopita ya kununua zao moja la mahindi peke yake.

Aidha Mgeja alisema kuwa uamuzi huo wa Serikali utakuwa mwarobaini wa kuwasaidia wakulima kupata bei nzuri katika mazao yao na kuwafanya wafanyabiashara wa mazao na baadhi ya walanguzi uchwara katika masoko nao watoe bei nzuri ya ushindani.

“Hivyo kumfanya mkulima anufaike na kilimo chake,kuna baadhi ya wakulima walianza kukata tamaa na kuchukua uamuzi mgumu wa kuachana na kilimo,” alisema 

Akizungumzia shamba lake, Mgeja alieleza msimu huu amelima ekari 73 na kuongeza kuwa lengo lake kuu ni kulima ekari 250 katika kipindi cha msimu ujao huku akifafanua mafanikio na changamoto zinazowakabili wakulima  kwa ujumla na kushindwa kufikia malengo ni kutokana na  miundo mbinu mibovu.

Hata hivyo amemshukuru Mungu kwa kuwapatia mvua na kwwmba kwa msimu huu anatarajia kuvuna magunia 1,430 ya mpunga na hadi sasa anaendelea kuvuna na amefikisha gunia 320.

Mgeja ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Shinyanga, alisema ameamua kupumzika siasa na mkkakati wake wa pili wa maisha yake amejielekeza kilimo na ufugaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles