23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mgeja atangaza ‘kupumzika’siasa

Mwandishi wetu

KADA maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja, ametangaza kupumzika siasa kwa muda na kujikita kwenye shughuli nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Kahama, Mgeja alisema kwa sasa akili yake ameielekeza katika shughuli za kilimo na michezo hasa soka la watoto wadogo.

“Mwalimu alitufundisha dhana ya siasa ni kilimo, nimeamua kujikita shambani    kumuenzi Mwalimu kwa vitendo na kuhamashisha vijana kujihusisha katika shughuli za kilimo zitakazowaongezea tija na kipato katika maisha yao.


“Hapa kwetu kilimo ni uti wa mgongo na ni kazi kama zilivyo kazi nyingine,  kwa kuwa Mwalimu alisema kazi ni kipimo cha utu basi nawahamasisha vijana waje shambani tuungane kujiletea maendeleo yetu,” alisema Mgeja.

Mgeja ni miongini mwa wanasiasa waliokumbwa na wimbi la Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, aliyehama CCM mwaka 205 na kujiunga na Chadema.

Alikuwa miongoni mwa waliohama na Lowassa ambako pia alishiriki kampeni za Chadema akimnadi Lowassa aliyepeperusha bendera ya Umoja wa Katiba (Ukawa), kupitia Chadema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles