29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mgambo atuhumiwa kukimbia na Sh 17.2/-

ABDALLAH AMIRI

KATIKA hali ya kushangaza mgambo mmoja aliyekuwa akikusanya ushuru wa fedha za maegesho ya malori mjini Igunga mkoani Tabora, Peter Hiiti Areray mkazi wa Mkoa wa Manyara anadaiwa kutoweka na fedha zote i.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli alithibitisha mgambo kukimbia na kiasi hicho alizokuwa amekusanya mwaka jana.

Alisema mgambo alirudisha mashine ya kukusanyia fedha katika halmashauri, akidai anakwenda kumuuguza mzazi wake nyumbani kwao Manyara.

Alisema pamoja na kumpigia simu ili arudi kwa ajili kurudisha fedha hizo, simu yake imebainika ameizimwa.

“Mgambo huyo tulimwamiani kwa sababu alikuwa mlinzi eneo la maegesho la malori, mwajiri wake wa halmashauri ya wilaya, tulijaribu kumwita mke wake ili atueleze mume wake alipokwenda, alisema amekimbia kwa sababu hana uwezo wa kulipa fedha hizo, huku akidai fedha hizo hakuchukua mume wake, bali kuna mhasibu aliyekuwa akizichukua akimjulisha anazipeleka benki.

Alisema kwa wale wengine waliokula fedha, wamepewa siku 14 wawe wamerejesha fedha zote na ambaye atashindwa kurejesha atafikishwa mahakamani.

Nae mmoja wa watumishi ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema katika idara ya uhasibu na biashara kuna fedha nyingi zimeliwa ambapo majina ya waliokula hayajapelekwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kunahitajika uchunguzi wa hali ya juu katika maeneo hayo mawili.

Alipotafutwa mgambo huyo, Peter Hiiti Areray kwa njia alisema yeye hajala fedha hizo kwani zote alikuwa akiwapa baadhi ya wahasibu ili wazipeleke benki 

“Mimi sijala fedha hizo, hawa wahasibu wananiingiza mimi kwenye matatizo kwa kuwa fedha zote shilingi milioni 17, 253,000, niliwakabidhi kwa nyakati tofauti.” Alisema Serikali inatakiwa kufanya uchunguzi wa kina au kuwahamisha baadhi ya wahasibu kwani fedha nyingi zimeishia mikononi mwao, nakuomba wewe mwandishi usinipigie simu tena alisema.

Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Igunga,Fransis Nzuakuu alisema wanaendelea kumtafuta mgambo huyo ili alejesha fedha hizo huku akisema hata kuwa tayari kuona fedha za serikali na wananchi zikiliwa hovyo pasipo kufanya shughuli za maendeleo kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles