31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mgambo 154 wahitimu mafunzo Jeshi la Akiba

Mohamed Hamad, Kiteto

Watu 154 ambao kati yao 13 ni wanawake, wamehitimu mafunzo ya Jeshi la akiba (Mgambo) Kijiji cha Ndaleta wilayaniKiteto mkoani Manyara na kutakiwa kukabiliana na vitendo vya uhalifu uliokithiri.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa, akizungumza na wahitimu hao leo Jumanne Desemba 18, amewataka kutambua kuwa serikali inatambua uwepo wao na kuwataka waanze kukabiliana na vitendo vya kihalifu.

“Ndaleta ni eneo lililokithiri kwa vitendo vya kihalifu, ninyi jeshi la akiba mtakuwa msaada mkubwa kwetu kukabiliana uhalifu huu,” amesema Magesa.

Akizungumzia ajira mkuu huyo wa wilaya amewataka wahitimu hao kutambua kuwa fursa ziko nyingi na kuwataka kuwa na nidhamu na kuepuka vitendo viovu.

Akisoma risala ya wahitimu, Jamali Kiondo, kwa niaba ya  wahitimu wenzake walimwomba mkuu huyo wa wilaya kuwapa kipaumbele katika ajira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles