24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mfungwa wa kisiasa afia jela kwa mateso

CAIRO, MISRI

JUMUIYA za kutetea Haki za Binadamu nchini Misri zimetangaza kuwa, mfungwa mwingine wa kisiasa, Muhandisi Hisham Abu Ali amefia jela akiwa chini ya mateso ya maofisa usalama wa nchi hiyo.

Jumuiya hizo zimeripoti kuwa, mfungwa huyo wa kisiasa ameaga dunia wakati alipokuwa akipewa mateso ndani ya makao makuu ya Shirika la Usalama wa Taifa la Misri katika mji wa Shibin El Kom, yalipo makao makuu ya Mkoa wa Monufia. 

Ripoti hiyo iliongeza kuwa, idadi ya wafungwa wa kisiasa waliofia mahabusu nchini Misri tangu Alhamisi iliyopita imefikia watu watatu.

Taasisi ya Haki na Uhuru ya Misri imetangaza kwamba Muhandisi Ali aliaga dunia akiwa chini ya mateso ndani ya makao ya Shirika la Usalama wa Taifa katika mji wa Shibin El Kom mkoani Monufia.

Taasisi hiyo ilisema Ali alikuwa miongoni mwa wanaharakati wa kisiasa wenye ushawishi mkubwa nchini Misri na kuongeza kuwa, alitoweka kwa kipindi cha wiki mbili na baadaye akaachiwa huru kisha akakamatwa tena na Shirika la Usalama wa Taifa. 

Familia ya mwanaharakati huyo wa kisiasa imesema maofisa wa Shirika la Usalama wa Taifa waliwapigia simu wakiwataka kwenda kuchukua maiti yake. 

Familia hiyo ilisisitiza kuwa kabla ya kutiwa nguvuni, Ali alikuwa mzima na mwenye afya nzuri na alikuwa hasumbuliwi na maradhi ya aina yoyote.

Subhi Fathi Abdel-Samad Ramadan maarufu kwa jila la Sobhi al Banna na Hamdi Abduh Hashim Abdel Barr ni wafugwa wengine wa kisiasa walioaga dunia wakiwa mahabusu siku ya Alhamisi wiki iliyopita.

Maelfu ya wafungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa mahabusu na gerezani nchini Misri wanasumbuliwa na mateso, kutelekezwa na kunyimwa huduma za matibabu.

 Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa jela na mahabusu za Msri zimegeuka na kuwa kama makaburi ya umati tangu baada ya mapinduzi ya Juni 2013, yaliyomuondoa madarakani rais wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kwa njia za kidemokrasia, Muhammad Morsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles