27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mfumuko wa bei watajwa kuongezeka Zanzibar

Khamis Sharif -Mjini Magharibi

MTAKWIMU kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Khamis Abdul-rahman Msham, amesema mfumuko wa bei umeongezeka kwa asilimia 2.2 kwa Septemba mwaka huu.

Alisema mfumuko huo umeongezeka ukilinganisha na Agosti mwaka huu ambao ulikuwa 2.1.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Unguja, Msham alisema kushuka kwa baadhi ya bidhaa muhimu nchini   kumesababisha kushuka kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 0.8 kwa Agosti kulinganisha na asilimia 1.2 kwa Septemba mwaka huu.

Alisema kuwa upande wa bidhaa hizo ikiwemo samaki wameshuka kwa asilimia 3.1, tan rice 2.5,  ndizi za Mtwike 4.7, mchele wa Mbeya 1.9 na sukari 0.3.

Naye Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (Suza), Dk. Suleiman Msaraka, alisema kuwa mabadiliko ya faharisi za bei yanaendana na wakati uliopo kwa kulinganisha na kipato cha wananchi.

“Bado tupo katika hali nzuri kama ilivyokadiriwa na Serikali, kwani ni baadhi ya vitu tu ambavyo vimeongezeka, lakini kwa bidhaa za chakula na viungo bado afadhali,” alisema Dk. Msaraka. Meneja wa Uchumi Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Zanzibar,  Moto Lugobi, alisema mfumuko umeongezeka na kwa upande wa soko la Zanzibar bado liko vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles