31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mfumuko wa bei washuka

RAMADHAN HASSAN – DODOMA

MFUMUKO wa bei kwa mwaka  ulioishia Agosti 2019 umepungua hadi  kufikia asilimia 3.6 kutoka  asilimia 3.7 Julai 2019.

Hayo yalielezwa juzi jijini hapa na Mkurugenzi wa Sensa  za Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Davison, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema mfumuko wa bei wa taifa unapima kiwango cha  kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

“Hii inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia  Agoati 2019 umepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo Julai 2019,” alisema. 

Alizitaja baadhi  ya  bidhaa  zisizo  za  vyakula zilizopungua  bei  kwa  Agosti 2019 zikilinganishwa  na bei za Agosti mwaka jana ni pamoja  na mafuta ya taa  kwa  asilimia 2.6, petroli  kwa asilimia 4.3, maji ya gesi kwa asilimia 1.4, gharama za kufanya ukarabati wa nyumba kwa asilimia 1.7 na bidhaa za usafi binafsi kama mafuta ya nywele kwa asilimia 1.3.

Alisema  kwa  upande  wa mfumuko  wa  bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti 2019, umeongezeka hadi  kufikia asilimia 3.7 kutoka asilimia 2.9 Julai 2019.

Pia alitaja hali ya mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo alisema nchini Kenya kwa mwaka ulioishia Agosti 2019 umepungua hadi asilimia 5.00 kutoka asilimia 6.27 kwa mwaka ulioishia Julai 2019.

Kwa upande  wa Uganda, mfumuko  wa  bei kwa mwaka ulioishia Agosti 2019 umepungua hadi asilimia 2.1 kutoka asilimia 2.6 kwa mwaka ulioishia Julai 2019.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles