25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mfumuko wa bei wapungua, nafaka na kakao zajitokeza mauzo nje

mahindi-ghalaniNa Joseph Lino

MFUMKO wa Bei  Septemba mwaka huu umepungua  kwa asilimia pointi 4 na kuwa  asilimia 4.5 Septemba kutoka asilimia 4.9  ilivyokuwa Agosti  mwaka huu.

Hii inamaanisha kuwa  kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia  Septemba, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Agosti,  mwaka huu. Ni punguko dogo lakini  ni muhimu kwa serikali iliyoko madarakani  kwa kudhibiti  matumizi  kwa serikali.

Mfumuko wa bei kwenye vyakula na vinywaji baridi mwezi Septemba mwaka  huu  ulipungua kwa asilimia 6.0 kutoka asilimia 7. Agosti mwaka huu.

Ripoti ya mfumuko wa bei ya  Septemba mwaka huu inaonesha  kuwa mfumuko wa bei wa vyakula vinavyotumiwa nyumbani na nje ya nyumbani ulipungua  na kufikia asilimia 6.1 katika Septemba  kutoka  asilimia 7 Agosti  mwaka huu.

Mfumuko wa Bei, ukiondoa chakula na nishati, ulipungua kwa asilimia  2.4 Septemba, ikilinganishwa asilimia  2.6  Agosti mwaka huu na  hivyo kufanya  ununuzi wa shilingi 100 za Tanzania kufikiwa shilingi 97 na senti 04 katika Septemba 2016 kuanzia Desemba 2015. Ilikuwa TZS96 na 83 senti mwezi Agosti 2016. Ina maana shilingi ya Tanzania iliongezeka thamani dhidi ya fedha nyingine na hivyo kufanya watu kulalama kuwa hakuna fedha mifukoni.

Katika thamani ya Sh.100 katika kununua bidhaa na huduma  umefikia Sh. 97 na senti 04 mwezi Septemba, 2016 kutoka Desemba mwaka jana,  ilipokuwa Sh.96 na senti 83 mwezi Agosti mwaka huu.

Mfumuko wa bei unazidi  kubadilika kwa kupanda na kushuka kutoka asilimia 6.8  Desemba mwaka jana,  Aprili mwaka huu mfumuko ulishuka  hadi kufikia asilimia 5.1, na ukaongezeka hadi asilimia 5.5 Juni mwaka huu, na kushuka tena  na kuwa asilimia 5.1 Julai, asilimia 4.9 Agosti na asilimia 4.5 Septembi  mwaka huu.

Kwa upande wa ripoti ya uchumi ya  Benki Kuu  (BOT) ya  Agosti mwaka huu inaonesha thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma katika mwaka unaoishia Julai mwaka huu , yaliongezeka kwa asilimia 7.5.

Ripoti hiyo inaelezea mauzo ya nje kwa ujumla yalifikia  dola za kimarekani milioni 9.810.4, ikilinganishwa na dola milioni 9,128.4 katika mwaka ulioisha Julai  mwaka jana.

Mabadiliko hayo yalitokana na ongezeko  katika  sekta ya utalii, bidhaa za viwandani, na dhahabu.

Sekta ya utalii  ni miongoni mwa  sekta iliyoongoza katika kuleta fedha za kigeni na bidhaa za viwandani, dhahabu, na mauzo ya bidhaa asilia.

Mapato ya fedha za kigeni kutoka bidhaa za viwandani iliongezeka kwa asilimia12.6 kufikia  dola za kimarekani milioni 1,448.7 kwa mwaka ulioisha Julai mwaka huu.

Ongezeko hilo nikutokana na maboresho ya  sekta  katika mavazi nguo (textile), mafuta ya kula, vitu vya plastiki, chuma na bidhaa za chuma.

Ripoti hiyo inaelezea pia mauzo ya nje ya madini ya dhahabu  iliongezeka kwa asilimia 7.7 kufikia dola za kimarekani  milioni 1,364.4 hili ni kutokana  ongezeka la kiwango cha  kuuza nje.

Miongoni mwa mauzo ya nje kwa  bidhaa za ndani  zilizoongezeka ni kama kahawa (dola milioni 151.8 ambayo ni kwa  aslimia 1.3), chai (dola 48.8 asilimia10.2), karafuu (dola  milioni 46.2 asilimia 52.5) na mkonge (dola milioni 25.7 40.4 ).

Pia kulikuwa na kupanda kwa thamani ya mauzo ya nje mafuta yanayotokana na mbegu za mazao, malighafi ya ngozi na kakao, nafaka, na bidhaa za mbao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles