23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mfumuko wa bei wapanda kwa asilimia 3.6

Ramadhan Hassan -Dodoma

MFUMUKO wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia Oktoba, mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 3.6 kutoka 3.4 kwa mwaka ulioishia Septemba, mwaka huu.

Hayo yalielezwa jijini Dodoma jana na Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Takwimu, Ruth Davison alipozungumza na waandishi wa habari.

Ruth alisema hali hiyo inamaanisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba, imeongezeka ikilinganishwa na iliyokuwepo.

Alisema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kumechangiwa hasa na kuongezeka bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia Oktoba, mwaka huu, zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba, mwaka jana.

Alizitaja baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoongezeka bei kuwa ni mchele kwa asilimia 6.1, unga wa mahindi (20.5), unga wa muhogo (10.9), nyama (2.2), samaki (16.4), maziwa ya ng’ombe (3.6), mafuta ya kupikia (7.0) ma maharagwe asilimia 4.9.

Alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia Oktoba, mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 5.1 kutoka 4.0 kwa mwaka ulioishia Septemba.

Ruth alisema hali ya mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki, nchini Kenya kwa mwaka ulioishia Oktoba, mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 4.95 kutoka 3.83 kwa mwaka ulioishia Septemba.

 “Uganda mfumuko ulioishia Oktoba 2019 umeongezeka hadi asilimia 2.5 kutoka asilimia 1.9 kwa mwaka ulioishia Septemba, mwaka huu,” alisema Ruth.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles