23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MEYA WA JIJI LA TANGA AWAONYA MADIWANI KUSHAWISHI WANANCHI KUKATAA MIRADI

Mwandishi Wetu, Dodoma             |               


Meya wa Jiji la Tanga, Mhina Mustapha amewaonya baadhi ya madiwani wa Jiji hilo kuacha tabia ya kuhamasisha wananchi kukataa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zao na badala yake washirikiane na wataalamu kutekeleza miradi hiyo kwa ubora.

Akizungumza wakati akifunga kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji hilo, leo Jumatano Septemba 5, amesema miradi mingi ya maendeleo katika Jiji hilo imekuwa na changamoto nyingi kutokana na baadhi ya madiwani kutotambua wajibu na mipaka yao na hivyo kuwahamasisha wananchi wakatae maendeleo.

Amesema kuna taarifa kwamba baadhi ya madiwani wamekuwa wakihamasisha wananchi wakae miradi kutokana na sababu za kisiasa hatua ambayo aliielezea kwamba haina msingi kwa sababu ni kukiuka taratibu kwavile miradi hiyo inatekelezwa kutokana na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Mheshimiwa diwani ni msimamizi wa shughuli za maendeleo na mwenyekiti wa kamati ya maendeleo, naomba tutambue mipaka yetu, lakini inafika mahali diwani unahamasisha wananchi wakatae miradi ya maendeleo kishabiki au kisiasa, fedha zile ni za serikali na miradi inatekelezwa kutokana na ilani ya CCM,” amesema.

Amesema katika miradi hiyo inayotekelezwa katika kata zao haitaandikwa majina ya madiwani bali inatekelezwa kwa mujibu wa taratibu na mipango iliyowekwa kuwaleteas maendeleo wananchi katika maeneo hayo.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Jiji hilo Daud Mayeji, amesema kuna kamati ya timu ya wataalamu inakutana kwa pamoja kwa ajili ya kutafuta namna bora ya Jiji la Tanga na halmashauri ya Mkinga watakavyonufaika na viwanda vya saruji vinavyojenga katika Kijiji cha Mtimbwani wilaya Mkinga.

Mayeji alikuwa akitoa ufafanuzi baada ya diwani wa kata ya Mawezi Joseph Colvas aliyetaka kujua namna halmashauri itakavyonufaika na kiwanda cha saruji kinachojengwa Mtimbwa wilayani Mkinga huku malighafi wakichukua katika Jiji hilo.

Mkurugenzi amesema kuna timu ya wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga, Mkinga na Jiji wanakutana kutafuta namna bora ya utaratibu utakaotumika katika kupata ushuru wa huduma ‘Service Levy’ kwa halmashauri hizo mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles