24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

MESSI, RONALDO, NEYMAR NANI MCHEZAJI BORA WA MWAKA?

LONDON, ENGLAND

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), limetoa orodha ya majina matatu ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ambao ni Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Neymar.

Viongozi wa Fifa na baadhi ya wachezaji wa zamani wa soka kama vile Roberto Di Matteo, Jay Jay Okocha, Peter Shilton, walikuwa miongoni mwa wageni waliokuwepo kwenye ukumbi wa The Bloomsbury Ballroom, uliopo jijini London nchini England, wakati wa kutangaza majina hayo.

Wageni wengine ambao walikuwepo wakati wa kutajwa orodha hiyo ni pamoja na beki wa kati wa klabu ya wanawake ya Arsenal, Alex Scott pamoja na mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Andre Shevchenko.

Hata hivyo, tuzo hiyo inatarajiwa kutolewa mwezi ujao katika makao makuu ya soka duniani, Zurich nchini Uswisi.

Msimu uliopita mshambuliaji wa Real Madrid, Ronaldo alitwaa tuzo hiyo baada ya kuisaidia klabu hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu nchini Hispania pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya, hata hivyo msimu huu anaonekana kupewa nafasi kubwa ya kuchukua tena tuzo hiyo.

Hata hivyo, orodha nyingine ambayo imetolewa na Fifa ni pamoja na tuzo ya mchezaji bora kwa upande wa wanawake, kocha bora kwa klabu za wanaume, kocha upande wa wanawake, mlinda mlango bora, goli bora la mwaka, pamoja na mashabiki bora.

Kwa upande wa walinda mlango ambao wanawania tuzo hiyo ni pamoja na Gianluigi Buffon, Keylor Navas pamoja na Manuel Neuer, lakini mashabiki wengi wameshangazwa na kuachwa kwa kipa wa Manchester United, David De Gea.

Kwa upande wa makocha ni pamoja na Zinedine Zidane wa Real Madrid, Antonio Conte wa Chelsea na Massimilliano Allegri wa Juventus.

Wachezaji bora kwa wanawake ni Deyna Castellanos, Carli Lloyd na Lieke Martens, huku makocha kwa upande wa wanawake ni Nils Nielsen, Gerard Precheur, Sarina Wiegman. Wakati huo tuzo ya bao bora ni Kevin-Prince Boateng, Alejandro Camargo, Deyna Castellanos, Moussa Dembele, Olivier Giroud. Aviles Hurtado, Mario Mandzukic, Oscarine Masuluke, Nemanja Matic na Jordi Mboula.

Tuzo kwa mashabiki ni wa klabu ya Borussia Dortmund, mashabiki wa Celtic na wa FC Copenhagen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles