30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MDEE, MNYIKA NA WAZIRI JENISTA WANYUKANA BUNGENI

Na ELIZABETH HOMBO-DODOMA


MJADALA kuhusu zilipo Sh trilioni 1.5, umeibuliwa bungeni jana na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliochangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Kwa dakika zipatazo 30 ukumbi ulitawaliwa na zomeazomea baada ya Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kuibua mjadala huo, hali iliyomlazimu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuingilia kati kwa kuendesha kikao ambacho awali kiliongozwa na Mwenyekiti, Najma Giga.

Akianza kuchangia mjadala huo jana, Mnyika aliitaka Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu zilipo Sh trilioni 1.5 ambazo alidai hazijulikani zilipo kama ilivyoelezwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mnyika alimtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kujiuzulu nafasi hiyo akidai ameshindwa kufanya kazi na huenda akawa waziri wa fedheha.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na kawaida ya Wizara ya Fedha kutoa kauli za mashaka ambazo hazipaswi kuaminika.

“Kwa mfano, Aprili 20 mwaka huu, ndani ya Bunge hili, Naibu Waziri wa Fedha, alitoa kauli akifafanua kuhusu utata wa Sh trilioni 1.5, akalieleza Bunge kuwa Sh bilioni 209 zimepelekwa Zanzibar.

“Nimefuatilia mjadala wa Baraza la Wawakilishi huko Zanzibar na ripoti za BoT, mpaka sasa hakuna anayeeleza hizo fedha zimepelekwa lini, akaunti gani na zilipelekwa namna gani.

“Kwakuwa naamini CAG ananisikia, basi uchunguzi ufanyike,” alisema Mnyika.

Kauli hiyo ya Mnyika, ilisababisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, asimame na kuomba kutoa taarifa.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles