27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mchungaji Msigwa: tunaanza mikutano 2020 kama Rais Magufuli alivyoagiza

FRANCIS  GODWIN-IRINGA

CHAMA  cha  Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) Kanda ya Nyasa  kimesema kimevumilia  na  kutekeleza kwa utii mkubwa agizo la  Rais Dk.  John Magufuli  la  kuzuia mikutano ya hadhara  ya  vyama  vya siasa  hadi mwaka 2020  wakati wa  kuelekea uchaguzi mkuu ambapo  sasa  wataanza  kazi ya ujenzi wa demokrasi kama  rais alivyoagiza .

Akizungumza na  wanahabari jana  mjini Iringa Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa  Mchungaji Peter  Msigwa ambae ni mbunge wa Iringa Mjini alisema  kuwa  chama chake  kimekuwa miongoni mwa vyama  vya upinzani nchini  ambavyo vilionyesha  utii  mkubwa wa utekelezaji wa agizo la Rais Dkt Magufuli kwa  kutofanya mikutano ya hadhara   kwa kipindi   chote cha miaka  minne  sasa.

Msigwa ambaye alikuwa ameambatana na  viongozi  wa kanda  hiyo, aliwataka viongozi wa wilaya na mikoa wa Chadema Kanda ya Nyasa  kuanza kuandaa mikutano  yao ya hadhara   kwa  kufuata  taratibu  zote za  kuomba  vibali  vya mikutano  hiyo  ili  kuendelea na ujenzi wa chama chao  kuelekea  Oktoba 25    siku ya  uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais .

” Tuliweza  kutekeleza agizo la mheshimiwa Rais  kwa utulivu  mkubwa japo  agizo hilo halikuwa  sawa maana  lilikuwa ni kinyume na makuzi ya  demokrasia  nchini,  vyama vya siasa msingi wake ni siasa  hivyo kuzuia  mikutano   kwa haikuwa sawa lakini  tuliweza  kutii.

“Ila  jamani si alisema hakuna  mikutano ya hadhara ya vyama  hadi mwaka 2020  na huu ndio  mwaka 2020  hivyo  tunaendelea na mikutano kama  kawaida ”  alisema mchungaji Msigwa .

Msigwa alisema miaka minne ambayo walizuiwa kufanya mikutano ya siasa chama hicho kanda ya  Nyasa   walikuwa  wakijijenga  zaidi  kuanzia ngazi za chini.

Alisema awali hawakuwahi kuwa na misingi hiyo na kwamba kwa sasa wana mtaji mkubwa kuliko hata  ilivyo kuwa  mwaka 2015 walivyoingia katika Uchaguzi Mkuu .

Alisema kuzuiwa kwa mikutano ya siasa ndiko kulikowapa nguvu ya kufanya vikao vyao vya ndani na kujengana  zaidi.

Alisema baada ya miaka minne bila  kufanya siasa   ya wazi   wanatoka wakiwa na mbinu na uwezo  wa kushindana  vikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akielezea kuhusu  hali ya  uchumi nchini  hasa kwa  mikoa ya Nyanda za  Juu Kusini  alisema kila mwananchi analia tofauti na ilivyokuwa Serikali ya  awamu ya tatu na ya nne.  

Aidha aliishutumu Serikali kwa kushindwa kusimamia  bei ya mazao  pia  kushindwa  kutafuta  masoko  nje  ya nchi   ili  kusaidia  wakulima  kulinda mitaji yao  jambo ambalo  limewaathiri   wakulima  hivyo  kupata hasara  kwa kuuza  mazao  kwa bei  za chini.

Akitolea  mfano  kwa  taarifa ya  Waziri wa Kilimo, Japhet  Hasunga  ya hali ya  uzalishaji  wa mazao ya chakula na upatikanaji wake taarifa ya mwaka 2018/2019   kuwa ilionesha     jumla ya  Halmashauri 46 katika  mikoa 13 zilikuwa  na upungufu wa chakula, miongoni  mwa  Halmashauri  hizo ni Halmashauri ya Iringa Vijijini ambayo ipo kwenye orodha ya kanda zinazozalisha  chakula kwa  wingi.

Kuhusu wafanyakazi wa umma, Mchungaji Msigwa   hawajaongezewa  mishahara  yao  kwa miaka minne  sasa   kinyume na sheria    huku gharama za maisha  zikiongezeka  siku  hadi siku.

Pia alisema  wafanyaakazi wa umma hawajapandishwa  madaraja  kinyume na sheria   kwa takribani miaka minne  sasa  tangu utawala  huu wa  wanyonge  uingie madarakani .

“Wafanyakazi waliostaafu ambao walitoa mchango mkubwa kwa Taifa  hadi sasa  malipo  ya pesheni  zao yamekuwa yakisua sua sana huku Serikali  ikijinadi  fedha  zipo  na tumeshuhudia  awamu  hii ya tano wafanyakazi wengi wa sekta  binafsi wamefutwa kazi  kutokana  na mazingira magumu katika  sekta  binafsi.”

Mchungaji Msigwa  alisema hali ya afya   kwa mwaka 211 katika maadhimisho ya siku ya wazee  duniani iliyofanyika mjini Morogoro   serikali ya CCM ilitangaza  kutoa  matibabu  bure kwa  wazee  jambo ambalo takribani miaka  9 sasa  wameshindwa  kulitekeleza.

Aidha  kuhusu elimu alitaja sababu sita  ambazo zinafanya  wanafunzi kuhangaika  ikiwemo ya mabadiliko ya  mara kwa mara ya sera ya  elimu  ya msingi, suala la mikopo ya  elimu ya juu na  sababu nyingine  ambazo wao  wamekuja na majibu .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles