28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mchungaji Msigwa atolewa bungeni JPM akipongeza kwa ‘kununua korosho’

Fredy Azzah, Dodoma



Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), ametolewa nje ya ukumbi wa Bunge, wakati Bunge likijadili azimilio lililowasilishwa bungeni na Mbunge wa Singida Magharibi (CCM), Elibariki Kingu, la kumpongeza Rais John Magufulu kwa hatua aliyochukua juu ya kununua zao korosho.

Chanzo cha kutolewa nje Msigwa ilikuwa ni mchango wa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Jackline Ngonyani, ambaye alikuwa akichangia azimio hilo huku akiwaponda wapinzani.

Katika mchango wake alisema wapinzani wamekuwa mabingwa wa kupinga kila kitu kuanzia suala la makinikia na hata Mradi wa Umeme wa Mto Rufiji.

“Wakati wa suala la makinikia wapo tuliokuwa tunawaona wanazunguka hotelini huko kupanga mikakati ya kukwamisha, hoja ya kutengeneza umeme wa Mto Rufiji pia walipinga,” amesema.

Wakati Ngonyani akisema hayo, Msigwa alisimama akawa anazungumza jambo lilofanya Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, kumtaka akae bila bafanikio.

“Msigwa wewe ni mchungaji, unajua kabisa Biblia inasema tuheshimu mamlaka mimi nazungumza wewe keti,” alisema.

Baada ya kujaribu kumsihi kwa muda bila mafanikio, alimuamuru kutoka nje, na alipokataa aliagiza askari wa bunge kumtoa nje.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles