27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘Mchongo’wazidi kuzoa washindi Coca Cola

Na MWANDISHI WETU – MWANZA

WAKAZI wa Kanda ya Ziwa na mikoa jirani mambo yanazidi kuwanyookea kwa kuendelea kujishindia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya Coca-Cola ijulikanayo kama ‘Mchongo chini ya kizibo’.

Zawadi hizo ni pamoja na pikipiki, televisheni bapa za kisasa, fedha taslimu na zawadi nyinginezo.

Wiki iliyopita washindi wa pikipiki 6 walikabidhiwa  zawadi zao sambamba na washindi wawili wa televisheni na wengine wengi waliojishindia fedha taslimu na fulana kutoka Kampuni ya Coca-Cola.

Waliokabidhiwa pikipiki ni Derick Magnus (Nyakato), Ismail Hamis (Magu),  Joseph Mafuru (Mahina Mwanza) Pendo (Bariadi Mkoani Simiyu), Daniel Keheta (Mkolani),na Marysiana Kijita (Hungumalwa).Waliokabidhiwa  televisheni ni Rhoda Joel, Marco Kitula.

Wakizungumza kwa furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi hao waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye lengo la kuinua maisha ya wateja wake

“Nimefurahi kujipata ushindi wa pikipiki  kutoka Coca-Cola nitaitumia katika shughuli za biashara ili kuongeza kipato cha familia  yangu”.alisema Marysiana Kijita ambaye ni mmoja wa washindi.

Derick Magnus alisema kuwa amefurahi kujishindia zawadi ya pikipiki kupitia promosheni ya ‘Mchongo Chini ya  Kizibo’na kudai kuwa itamrahisishia usafiri wake binafsi na familia yake “Chombo hiki kitarahisisha usafari katika shughuli zangu za ujasiriamali sambamba na  usafiri kwa familia  yangu”.Alisema.

Mmoja wa washindi wa televisheni, Marco Kitula ,alisema kuwa zawadi aliyojishindia imekuja kwa wakati mwafaka ambapo ataweza kuona matukio mengi na michezo mbalimbali kupitia televisheni yake ya  kisasa aliyojishindia “Napenda sana kuangalia  matukio kupitia luninga na michezo mbalimbali nitaburudika vizuri na  familia na marafiki”.Alisema kwa furaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles