25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mchezo wa kuigiza wabadilisha tabia za vijana  

NA WINFRIDA NGONYANI

IMEELEZWA kwamba mchezo wa kuigiza wa shuga unaorushwa katika redio mbalimbali nchini umesaidia kubadilisha tabia za vijana hasa katika harakati za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi.

Mratibu wa mchezo huo, Pendo Laizer, alisema mchezo huo unalenga zaidi vijana hususani wasichana ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

Alisema ulianzishwa mwaka 2014 kwa ushirikiano kati ya MTV, HIV and AIDS Free Generation, Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef).

“Tumeanzisha programu mbalimbali za vipindi vinavyolenga kuelimisha jamii juu ya maambukizi ya VVU na matumizi sahihi ya kinga na kuepukana na msongo rika,” alisema Laizer.

Kwa mujibu wa mratibu huyo, baada ya mafanikio yaliyopatikana katika msimu wa kwanza, Tacaids na Unicef pamoja na wadau wengine walipanua wigo wa mradi huo kwa kuandaa vipindi zaidi vya kuelimisha jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles