24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mchezaji wa zamani Coastal kumrithi Mayanja

mayanjaNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Coastal Union unatarajia kumkabidhi majukumu ya timu hiyo mchezaji wake wa zamani, Mbwana Bushiri, baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Jackson Mayanja.

Kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kilichokutana juzi, kilifikia uamuzi wa kumtimua kocha huyo raia wa Uganda kutokana na timu hiyo kufanya vibaya katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea.

 

Abushiri aliyewahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na mwanachama wa klabu hiyo, ataanza rasmi kibarua cha kuinoa timu hiyo baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa jana katika Uwanja wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mayanja aliyeifundisha Kagera Sugar msimu uliopita, amefungashiwa virago Coastal Union baada ya kushindwa kuipatia timu hiyo matokeo ya ushindi tangu kuanza kwa ligi hiyo ambapo katika mechi saba zilizochezwa amefungwa mara nne na kupata sare moja.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Oscar Assenga, alisema Abushiri amekabidhiwa majukumu ya timu kutokana na uzoefu alionao kwenye soka ambapo pia alikuwa ni mshauri wa kamati ya ufundi ya timu.

Alisema lengo la mabadiliko hayo ni kutaka timu ipate matokeo mazuri Ligi Kuu na kuondoa aibu ya kutoshinda mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa ligi hiyo

“Pamoja na kuwa mwanachama wa Coastal kwa muda mrefu, Bushiri pia ana uzoefu mkubwa kwenye soka hivyo anakabidhiwa timu akisaidiana na viongozi wengine wa benchi la ufundi wakati mchakato wa kumpata kocha mpya ukiendelea,” alisema.

“Uongozi unaamini kuwa Bushiri ataisaidia timu kutoka kwenye hali mbaya tuliyonayo na kuinusuru na matokeo yasiyoridhisha baada ya kugundua udhaifu na kuufanyia kazi,” alisema.

Imeelezwa kuwa mwenendo mbaya wa timu hiyo umetokana na aina ya ufundishaji wa kocha huyo ambao ulikuwa haueleweki kwa wachezaji na kuchangia kuwaathiri na kucheza kwa kiwango cha chini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles