25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MCHELE, NYANYA WAPAISHA MFUMUKO WA BEI NCHINI

Baadhi ya bidhaa za vyakula zikiwamo mtama, nazi, nyanya, mihogo na mchele vimechangia ongezeko la mfumuko wa bei kwa asilimia 5.3 Septemba kutoka asilimia 5.0 Agosti, mwaka huu.

Aidha, uwezo wa sarafu ya shilingi 100 ya Tanzania, imekuwa na uwezo wa kununua bidhaa na huduma umefikia Sh 92 na senti 18 Septemba mwaka huu ikilinganishwa na Sh 92 na senti 20 ilivyokuwa Agosti, mwaka huu.

Takwimu zinaonyesha kuwa mtama umepanda kwa asilimia 19.8, nazi asilimia 14.8, nyanya asilimia 10.5, mihogo asilimia 11.5, na mchele asilimia 9.7.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) amewaambia waandishi wa habari leo kuwa kuongezeka kwa mfumuko huo wa bei umechangiwa na kupanda kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

“Aidha, baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mkaa asilimia 13.9, kodi za nyumba na makazi binafsi asilimia 6.3 na mabegi ya shule asilimia 9.4,” amesema.

Hata hivyo, amesema mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo Septemba mwaka huu nchini Uganda umeongezeka hadi asilimia 5.3 kutoka asilimia 5.2 Agosti, wakati nchini Kenya umepungua hadi asilimia 7.06 Septemba, kutoka asilimia 8.04 Agosti, 2017.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles