30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MBWA WA POLISI WAKODISHWA MITAANI

ZIARA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Susan Kolimba (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Avod Mmanda, wakitembelea kambi ya muda ya raia wa Msumbiji waliokimbia nchini mwao, eneo la Kivava, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara juzi. PICHA: FLORENCE SANAWA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM         |    


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema baadhi ya mbwa wa Jeshi la Polisi walioko katika Bandari ya Dar es Salaam, wanakodishwa kwa makampuni binafsi   Dar es Salaam na nje ya jiji hilo.

Aliyasema hayo jana alipozungumza na MTANZANIA kwa simu baada ya ziara yake katika Bandari ya Dar es Salaam aliyoifanya  kujua utendaji kazi wa bandari hiyo.

“Baada ya kufanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam leo (jana), kuna maagizo niliyatoa kutokana na taarifa nilizonazo kuhusu mbwa wa polisi.

“Taarifa nilizokuwa nazo ni kwamba  pale bandarini kulikuwa na daftari lililokuwa na mbwa 23 hadi kufikia Julai 16, mwaka huu.

“Lakini, katika mazingira ya kutatanisha, Julai 17, mwaka huu  lile daftari lililokuwa na idadi hiyo ya mbwa  liliachwa na wahusika wakaanzisha daftari jingine jipya ambalo linaonekana kuna mbwa 60.

“Katika utafiti wangu nimegundua wale mbwa baadhi yao wanakodishwa kwa watu binafsi na wengine kwenye makampuni binafsi wakati mbwa hao ni mali ya Serikali na wanatambulika kwa majina na wanalipwa posho za kuwatunza.

“Kibaya zaidi ni kwamba …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles