33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge: Waliouza viwanja mabondeni wakamatwe

MWITANA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Ukonga jijini Dar es Salaam, Mwita Waitara (Chadema),  ameitaka Serikali kuanza kuwachukulia hatua wale wote waliowauzia viwanja wananchi wa mabondeni, kwani hao ndio chanzo cha ujenzi wa makazi katika mikondo ya maji.

Pia ameitaka Serikali kuwachukulia hatua watendaji wa Halmashauri ya Ilala kwa kuwabomolea wananchi wanaoishi katika Bonde la Mto Msimbazi bila kuwapa notisi ya kujiandaa kuhama.

“Halmashauri hiyo kuna mapele makubwa ambayo yameiva na hayana haja ya kutumbuliwa bali yakiguswa yatatumbuka yenyewe…nafikiri ni muda mwafaka kwa Serikali kuanza kuyatumbua,” alisema.

Waitara alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo hilo kuhusiana na zoezi la ubomoaji  ambalo bado linaendelea katika halmashauri hiyo.

Alisema Serikali isiishie kuwabomolea wananchi  nyumba zao bali pia iangalie Manispaa ya Ilala kuna maeneo ya wazi ambayo yamechukuliwa na baadhi ya viongozi wa Serikali, hivyo ilipaswa kuyaangalia hayo kwanza kabla ya kuhamia kwa walala hoi.

“Kwa kweli Serikali ilitakiwa kuanza kubomoa maeneo yote ya wazi yaliyochukuliwa na wakubwa, hivyo kitendo cha kuwabomolea wananchi masikini kitaleta athari kubwa,” alisema Waitara.

Mchungaji mmoja aliyefahamika kwa jina la Mariam kutoka Bonde la Mto Msimbazi alihoji kuwa nani atahusika na kupima nyumba zinazotaka kubomolewa na ni nani atakayesimamia, maana hawana elimu ya kutosha juu ya kubomolewa nyumba zao.

“Baada ya sikukuu nitakutana na waathirika wote kisha nitaenda serikalini kuonyeshwa maeneo gani yanatakiwa kubomolewa na utaratibu ambao unatakiwa kufanyika katika maeneo yenu… lazima tuwe na waraka wa serikali na si kubomolewa holela.

“Inasikitisha hili zoezi la bomoabomoa limesababisha madhara makubwa kwa  wananchi kuwa na hisia tofauti ambazo zimepelekea wengi kupata maradhi mbalimbali ya ugonjwa wa moyo ni wakati sasa wa serikali kuanza kuwawajibisha hata wauzaji wa maeneo hayo,” alisema Waitara.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles