Mbunge Chadema atamani kuwa Waziri wa Magufuli

0
821

Arodia Peter, Dodoma

Mbunge wa Ndanda, Cecily Mwambe, (Chadema) amesema anatamani kuwa Naibu waziri wa Kilimo ili asaidie kuokoa zao la korosho ambalo limo kwenye matatizo makubwa.

Mwambe ameyasema hayo wakati akijadili hotuba ya Wizara ya Kilimo Bungeni leo, Mei 17, ambapo pamoja na mambo mengine amesema viongozi waliopo kwenye wizara hiyo wameshindwa kumshauri vizuri rais na hawana kauli nzuri kwa wadau wa korosho.

Amesema matatizo makubwa yaliyojitokeza kwenye ununuzi wa korosho ni matokeo ya viongozi hao kutokuwa na uwezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here