24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Chadema aeleza sababu kujiunga CCM

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


MBUNGE wa Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema), amejiuzulu ubunge na kujivua uanachama wa chama hicho, na kutangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Barua ya Gekul kujivua ubunge na uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani, ilisambaa katika mitandao ya  jamii juzi usiku ikionyesha kwenda kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Akizungumza na MTANZANIA kwa   simu jana, Gekul alikiri kujivua nyadhifa hizo na uanachama wa Chadema.

“Ni kweli hiyo barua inayosambaa ni ya kwangu na sababu za kujivua ziko humo, kwa mengine zaidi naomba unipigie baadaye kidogo,”alisema Gekul.

BARUA YAKE KWA SPIKA

Katika barua hiyo aliyoielekeza kwa Spika Ndugai, Gekul alianza kwa kuelezea historia yake ya siasa akisema safari yake ya kuwatumikia wananchi ilianza mwaka 2010, alipogombea ubunge kwa tiketi ya Chadema katika jimbo hilo la Babati Mjini.

Alisema katika uchaguzi huo alipata kura 7000 akimfuatia mbunge wa CCM aliyepata wastani wa kura 10,000 na idadi ya wapiga kura ikikaribia 19,000.

“Napenda ifahamike baada ya uchaguzi nilipata heshima ya kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema kwa mwaka 2010-2015.

“Mheshimiwa Spika, napenda ifahamike kwamba nikiwa Mbunge wa Mkoa wa Viti Maalumu  nimeshirikiana na wanachama wa Chadema Babati Mjini kujenga chama na kukiimarisha kuanzia ngazi ya msingi mpaka wilaya na mkoa.

“Mwaka 2014 nilipewa heshima na wanawake wa Chadema kuwa mwenyekiti Baraza la Wanawake (Bawacha) kwa Mkoa wa Manyara nafasi ambayo ninaishikilia hadi leo.

“Mwaka 2015 nikitambua nafasi ya viti maalumu ni fursa ya kujengewa uwezo nilijitoa nikashiriki uchaguzi wa jimbo.

“Haikuwa kazi rahisi, nimejifunza kufanya kazi kwa kujitegemea na kufanya kampeni za jimbo nikiwa mwanamke.

“Katika uchaguzi huo, wananchi wakanichagua kwa kura zaidi ya 21,000 nikifuatiwa na mgombea CCM aliyepata wastani wa kura 16,000 na mgombea wa ACT-Wazalendo akipata wastani wa kura 500.

“Mheshimiwa Spika, heshima niliyopewa na wananchi wa Babati Mjini ilinifanya niwe miongoni wa wabunge sita wanawake waliogombea na kushinda katika majimbo ya uchaguzi kupitia Chadema,”alisema Gekul.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles