MBUNGE ATAKA WILAYA YA TUNDURU IGAWANYWE

0
1005

Mwandishi Wetu, Dodoma           


Serikali imesema imesitisha uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala hadi yaliyopo yaimarishwe kikamilifu.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Josephat Kakunda, amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu Septemba 10, wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini, Daimu Mpakate ambaye alihoji mpango wa serikali kuigawa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Mtwara ambayo ina wilaya sita.

Akiuliza swali hilo bungeni jijini Dodoma jana, mbunge huyo amesema; “Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru iliomba kuigawa wilaya hiyo ambayo ni kubwa zaidi mkoani humo ikiwa na wilaya sita, kata 39 na vijiji 167, je serikali ina mpango gani wa kuigawa ili iwe rahisi katika kutoa huduma karibu zaidi na wananchi.”

Kajibu swali hilo, Kakunda amesema suala hilo lina changamoto ya kuimarisha kwanza miundombinu kama majengo ya ofisi, nyumba za watumishi na mahitaji mengine kama vifaa, watumishi wa kutosha na vyombo vya usafiri kwenye maeneo mapya ya utawala tangu mwaka 2010 na 2012.

“Maombi ya kugawa Wilaya ya Tunduru na kuanzisha Halmashauri ya Wilaya ya Busanda, yaliwasilishwa Tamisemi yakiwa na ombi la kuanzisha Mkoa mpya wa Selous. Serikali imetafakari maombi hayo na kuyaona ni ya msingi lakini yana changamoto nilizoainisha awali,” amesema Kakunda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here