MBUNGE ATAKA WANAOTAKA KUFANYA MAPENZI ‘CHAP CHAP’ WARUHUSIWE KUJIPIMA VVU WENYEWE

2
977

Mwandishi Wetu, Dodoma                             |                                


Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema), ameitaka Serikali kuruhusu watu kujipima wenyewe maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi(VVU) ili wanaotaka kufanya mapenzi haraka wafanye wakiwa na uhakika wako salama.

Akiuliza swali hilo bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Septemba 6, Lyimo alisema kwa sasa wananchi wana uelewa kuhusu masuala ya ugonjwa wa Ukimwi ambapo alitaka kujua ni kwa nini serikali hairuhusu watu kujipima wenyewe kwa kipimo cha haraka (Rapid HIV Test).

“Mwenyekiti ukienda Vituo vya Afya usiku vimefungwa na kuna watu wanataka kufanya ‘chap chap’ kwa nini wasiruhusiwe wafanye vipimo hivyo ili waende kwenye shughuli hiyo wakijua wako salama,” amehoji Lyimo.

Aijibu swali hilo, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema kwa mujibu wa Sheria ya Afya, upimaji unafanyika Kituo cha Afya lakininpia serikali imeanza mchakato wa sheria hiyo ili watu waweze kujipima wenyewe.

“Lakini kumeibuka mjadala kuna wengine wanasema mtu akijipima mwenyewe ataendabkuambukiza wengine.

“Kwa hiyo kwanza tutaanza kuruhusu mtu ajipime mwenyewe lakini mbele ya Ofisa wa Afya katika Kituo cha Afya, hayo ndiyo mapendekezo tuliyotoa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tutauleta bungeni ili wabunge mtusaidie,” amesema Mwalimu.

2 COMMENTS

  1. Swala la mtu kujipima mwenyewe ni zuri sana na inafaa sana kua hivo, lakini tuangale na upande wa pili madhara ya kisaikolojia (Psychological impacts) amvazo huyu mgonjwa atakaye bainika anamaambukizi ya VVU.

    Na ndio maana wataalam waka create HIV counseling and guidance, sasa huyu mtu anae jipima mwenyewe ushauri anaupata kwa nani? Matokeo yake atakua na msongo wa mawazo, ataamua kuusambaza kwa maksudi kitu ambacho ni hatari kwake yeye mwenyewe na kwajamii nzima inayo mzunguka.

    Mimi binafsi naiomba serikali isiruhusu kabisha hiyo sheria kwani tutapoteza watu wengi sana wengine watajiua wao wenyewe atakapo jigundua kua ni HIV+ na hana Psychological assistance.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here