MBUNGE ‘AIAMSHIA DUDE’ MITANDAO YA KIJAMII

0
35

 

DODOMA

Mtandao wa kijamii ya Instagram na Whatsapp, imezua jambo bungeni leo baada ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga ‘kuliamsha dude’ akidai mitandao hiyo mitandao hiyo inasababisha mmomonyoko wa maadili, uvunjifu wa sheria na katiba na kuhamasisha ngono.

Mbunge huyo akiomba mwongozo wa Spika baada ya kipindi cha maswali na majibu, ambapo ameitaja hiyo kuwa imekuwa ikihamasisha ngono na mapenzi ya jinsia moja na kitovu cha kutoa habari za uzushi.

“Mitandao hiyo imekuwa ikitoa habari za uzushi kwa mfano kuna mtu aliwahi kujiuzulu kupitia Instagram akasema amemwandikia barua Spika, imekuwa ikitoa taarifa ambazo zimekuwa zikizua taharuki katika nchi, wenyewe wanaita kuchamba, serikali imekuwa ikivuliwa nguo huko kwa kuchambwa.

‘Whatsapp ina makundi ya watu kutangza biashara za mapenzi ngono, kurusha picha za utupu na shuguli mbalimbali za kuharibu maadili ya nchi, Mheshimiwa Mwenyekiti nilikuwa naomba mwongozo wako kuhusiana na mitandao hiyo na mingine.

“Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lipi ni jukumu lao katika hili maana maadili yanaporomoka wanafunzi hao sasa hivi ukiwaangalia ni wakubwa kuliko mimi,” amesema Mlinga.

Akijibu suala hilo Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema serikali imeona jinsi kukua kwa teknolojia kunavyoweza kusababisha mmomonyoko wa maadili na kuahidi kulifanyia kazi.

“Serikali itaendelea kutolea ufafanuzi, maelekezo na ushauri wa kisheria kupitia sheria tulizo nazo kwa jinsi teknolojia inavyozidi kukua,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here