24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE AHOJI STARS KUFANYA VIBAYA KIMATAIFA

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

MBUNGE wa Kilolo,Venance Mwamoto (CCM), amehoji Serikali imechukua hatua gani  kuhusiana na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kufanya vibaya katika michezo ya kimataifa.

Akiuliza swali jana bungeni mjini Dodoma, Mwamoto alidai kuwa, timu ya Taifa imeendelea kufanya vibaya katika michezo ya kimataifa, hivyo Serikali imechukua hatua gani kuinusuru hali hiyo.

“Je, Serikali imeliona hilo na imechukua hatua gani,” aliuliza.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, alisema Serikali imekuwa ikifanya juhudi katika kuendeleza michezo, ili kuwa na timu bora za michezo katika ngazi mbalimbali.

Alisema baadhi ya juhudi hizo ni pamoja na kuboresha mazingira ili wadau wawekeze kisayansi katika michezo kwa kuanza na umri mdogo, kwa lengo la kugundua na kuendeleza vipaji.

Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay (CCM), alihoji kuhusiana na timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kwa sasa ipo wapi.

“Je, Wizara ina mpango gani kuwaendeleza vijana hao ili kutokuwa na ile kauli yetu ya zimamoto, pia waendelee kufanya vizuri.”

Akijibu swali hilo, Wambura alisema kwa sasa wachezaji hao wameunganishwa na majeshi na wanatunzwa na kituo cha JKT, ambapo hufanya mazoezi kila siku.

“Ni kweli Serengeti Boys imefanya vizuri na imetoa mfano katika timu za Taifa katika mashindano ya kimataifa, sisi kama Serikali kwa upande wa Wizara tulichokifanya ni kuwachukua vijana hawa.

“Tumewaunganisha na Majeshi na kwa sasa wanatunzwa katika kituo cha JKT na pale wanafanya mazoezi ya kila siku,” alisema Wambura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles