33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge ahamisha wananchi eneo la mauaji Tanga

Mbaruk+PHOTONa Amina Omari,TANGA

MBUNGE wa Tanga Mjini, Mussa Mbaruk (CUF), amelazimika kukatisha vikao vya Bunge vinavyoendelea   Dodoma na kwenda kuwahamisha wananchi wa   Kibatini yalipotokea mauji ya watu wanane.

Hatua hiyo ya mbunge huyo imekuja baada wananchi wa eneo hilo   kutaka wahamishwe katika eneo hilo wakihofia   maisha yao.

Mbunge huyo   alifika katika eneo hilo jana na na kukutana na    baadhi ya wananchi wakiwa wameanza kubeba mizigo yao kwa ajili ya kuhama.

Baada ya kusikia kilio hilo mbunge  alisema anaungana na wapiga kura wake akisema kwa sasa eneo hilo si salama kwa maisha .

Alisema wakati Serikali ikiendelea kutafuta wahalifu wa tukio hilo la kinyama ni vema  wananchi hasa wanaishi katika eneo hilo wakapatiwa msaada wa hali ya mali ikiwamo ulinzi wa uhakika jambo ambalo bado halijafanyika.

“Eneo hili kwa sasa si salama kutokana na mauaji ya kinyama yaliyofanyika huku ulinzi hadi sasa si wakuridhisha. “Sana sasa nami ninaungana nao wananchi hao ni bora kwanza waende eneo jingine kuliko hapa.

“Unajua linapotokea tukio kubwa na zito kama hili ambalo huwaathiri watu kisaikolojia huitajika juhudi za makusudi kuwasaidia maana sasa Tanga tumekuwa kama vile tuko katika nchi gani yailai!” alisema Mbaruk.

Alisema ni vema vyombo vya dola viwatafute wahalifu waliofanya unyama huu kwa vile  jiji la Tanga limekuwa likikumbwa na matukio ya ajabu yanayokwenda   kinyume na misingi ya haki za binadamu.

“Kutokana na matukio haya yanayoendelea hata uwekezaji katika jiji la Tanga unaweza kutiliwa  shaka au  ukaingia dosari kutokana na matukio hayo ya uhalifu ambayo yanaonyesha kuwa na sura ya ugaidi,” alisema.

Alisema  tukio hilo la mauaji linaonyesha kuwa kama lina dalili za visasi hivyo ni lazima vyombo vya usalama kuhakikisha vinamaliza matukio hayo ya uhalifu.

“Matukio yanayoendelea Tanga ni mtihani mkubwa kwa Serikali kwa sababu  katika kipindi cha mwezi wa tano pekee kuna matukio zaidi ya matatu ya uvamizi na mauaji yametokea,” alisema.

Akiwa katika eneo hilo baadhi ya wananchi walieleza hofu yao kuhusu usalama wao kutokana na kutoridhishwa na   kutokuwapo vyombo  vya ulinzi na wakati wote.

Akizungumzia hali hiyo mkazi wa eneo hilo, Malik Abdallah,  alisema ulinzi katika eneo hilo  hasa katika muda wa mchana ni tofauti na usiku.

“Usiku hatulali vizuri kwa sababu  kama jana (juzi) baada ya maziko ya ndugu zetu tulilazimika kulala nje na huku tukilindwa na vikosi vya Jeshi ambavyo viliondoka asubuhi,” alisema Abdallah.

Sheikh wa Mkoa

Sheikh wa Mkoa wa Tanga, Ali Juma Luuchu, aliiomba Serikali kushirikisha viongozi wa dini   na wazee   kutafuta suluhu ya kudumu ya matukio hayo yanaonekana kutamalaki katika jiji hilo.

Alisema  tukio hilo haliwezi kuachiwa serikali pekee kwa vile ni lazima wao kama viongozi wa dini washirikiane na kuhakikisha  vitendo hivyo vinatokomezwa kwa sababu vinachafua sura ya mkoa na nchi kwa ujumla.

Mji wa Tanga unasifika kwa kuwa na watu wakarimu na wenye imani hivyo   matukio hayo ya uhalifu yanaiharibu sura nzuri ya mji huo, alisema.

Akizungumzia tukio hilo kuhusishwa na imani za dini, alisema   hakuna dini yoyote duniani inayohamasisha machafuko   na mauaji bali dini zinahamasisha upendo na ushirikiano miongoni mwa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles