30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MBOWE: HATUSOMI HOTUBA, HATUSUSI BUNGE NG’O

Na Fredy Azzah, Dodoma

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), imesema haitasoma hotuba wala taarifa zake bungeni endapo utaratibu wa kuziwasilisha kwa Katibu wa Bunge hatua ya kuhaririwa kwanza kabla ya kusomwa bungeni itaendelea.

Pamoja na hayo, wamesema hawatatusa bunge kwa ajili hiyo wala sababu nyingine yoyote.

Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema hayo leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mustakabali wa wabunge hao kuhudhuria vikao vya bunge na kuhusu kukataliwa kusomwa kwa hotuba yao bungeni leo.

Mbowe amesema anamshangaa Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kukataa kutosomwa kwa taarifa ya kambi hiyo bungeni leo kwa sababu tu haikuwasilishwa kwa Spika siku moja kabla ya kusomwa bungeni.

“Naibu Spika anasema hotuba ya KUB haipo wakati anajua kambi ilikuwa ina watumishi wanne ambao walikuwa wanafanya utafiti, kuandaa randama ya serikali, kuandaa hotuba zote zikiwamo za serikali sasa watumishi hao tangu Desemba mikataba yao iliisha na niliandika dokezo kuomba wapewe mkataba upya hadi sasa Katibu wa Bunge amekataa kufanya hivyo akidai Spika wa Bunge yuko nje kwa matibabu.

“Sawa walitaka hotuba hiyo niiandikie Segerea, kwa sababu wale vijana ndiyo walikuwa wakifanya hayo na bunge lina watumishi wa mikataba 30 wakiwamo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wote wana mikataba ya miaka miwili miwili lakini wengie wako ofisini isipokuwa wa kambi ya upinzani ambao walikufukuzwa kama mbwa katika bunge la Januari,” amesema Mbowe.

Pamoja na mambo mengine, Mbowe amesema hapatakuwa n ahotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni hadi watumishi wa warejeshwe lakini pia hata watakaporejeshwa, hawatakuwa tayari kupeleka hotuba zao kwa katibu wa Bunge akachague ni nini cha kusoma bungeni na nini cha kuacha na kwamba Bunge liking’ang’ania kufanya hivyo, hawatasoma hotuba hizo.

Akizungumzia suala hilo, Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai alisema bunge lina watumishi wa kutosha kuhudumia wabunge na ofisi zao.

Alisema hadhani kama aliyozungumza Mbowe yatakuwa na ukweli wowote kwa sababu bunge linahudumiwa na Sekretarieti ya Bunge na watumishi wake walioajiriwa na kuhudumia wabunge.

“Hatujakosa sekretarieti, nina watumishi wa kutosha kuhudumia wabunge.

Kulikuwa na watumishi wa mkataba ambao mkataba wao ulimalizika Desemba, sasa alitakiwa kusema kama anawahitaji hao lakini mwenye uwezo wa kusema waendelee au wasiendelee ni Tume ya Utumishi wa Bunge.

“Kwangu alikuja akaniambia lakini sasa mimi ni mtumishi wa Bunge na kama unavyofahamu Spika wa Bunge alikuwa nje kwa matibabu.

“Watumishi walioajiriwa na Bunge wapo, mimi nikiwa mmojawapo kama mbunge anawahitaji anapewa lakini si kwa kazi binafsi. Kama anataka watumishi wa bunge kumhudumia yeye peke yake hiyo ni juu yake, wanaweza kuwa hawataki lakini sisi hatuwezi kuwalazimisha,” amesema Kagaigai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles