23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mbowe amtaka Magufuli kuwawajibisha wahusika ajali ya MV Nyerere

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam     



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemtaka Rais John Magufuli, kuwawajibisha waliohusika kwa namna moja ama nyingine kusababisha ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere, iliyotokea jana Ukerewe mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Septemba 21, Mbowe amesema Rais Magufuli achukue hatua hiyo haraka kwani amewawajibisha watu wengi kwa sababu mbalimbali kwenye hili pia afanye hivyo.

“Na asiseme hachukui hatua kwa sababu amesema Mbowe, hili ni suala la kitaifa ndugu zetu wamefariki, ni msiba wetu.

“Huu ni msiba wa kitaifa tunamtaka Rais Magufuli pia azungumze na taifa, isitoshe tu Msigwa wa Ikulu (Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa) kutoa taarifa TBC kwamba rais anatoa pole, azungumze na Watanzania awape pole tunaamini atautambua ni msiba wa taifa na atangaze maombolezo,” amesema Mbowe.

Aidha, amesema serikali ijiandae fidia kwani utaratibu wa kawaida wa vyombo vya usafiri vinakatiwa bima na kwamba kivuko kile lazima kimekatiwa kwani ni kivuko kinachobeba roho za watu hivyo ni lazima watengenezewe utaratibu wa bima ili wanapopoteza maisha familia zao lazima zilipwe fidia lakini kwa sababu hakuna watu wanaowajibika utaratibu huo haufanyiki.

“Sisi kama chama tutashiriki kuomboleza katika msiba huu tunasubiri taarifa kama kutakuwa na mazishi ya halaiki au misa maalumu, tunasubiri kwa unyenyekevu tuungane kuwasindikiza wenzetu hawa ambao wametangulizwa mbele ya haki kwa uzembe wa watu wachache,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles