33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mbinu kupunguza vifo vya uzazi zatajwa

TUNU NASSOR

-Dar es Salaam

VIFO vitokanavyo na uzazi vinaweza kupungua kutoka vifo 556 kwa kila vizazi 100,000 hadi 292 iwapo kutakuwa na uwekezaji wa kutosha katika uzazi wa mpango.

Hayo yamesemwa na Meneja Utetezi kutoka mradi wa Advance Family Planning, James Mlali, alipowasilisha mada katika mafunzo ya waandishi wa habari juzi.

Alisema changamoto iliyopo ni kutokupelekwa kwa wakati fedha za bajeti zinazopangwa kwa sekta hiyo.

“Tunaiomba Serikali kuhakikisha inapeleka kwa wakati bajeti inayopangwa katika uzazi wa mpango ili huduma zitolewe kwa kiwango kilicho bora,” alisema Mlali.

Alisema  kwa mujibu wa takwimu, Mkoa wa Geita unaongoza kwa kutokutumia njia za uzazi wa mpango.

Aliongeza kuwa uwekezaji zaidi katika afya ya uzazi wa mpango utasaidia kupunguza mimba za utotoni kutoka 1,006 hadi kufikia 72 kwa mwaka.

“Hii itasaidia kuwapo kwa chakula cha kutosha kwa kuwa hadi sasa zaidi ya asilimia 54 ya Watanzania hawapati chakula mara tatu kwa siku,” alisema Mlali.

Naye Ofisa Utetezi, Halima Sharriff alisema kuwekeza zaidi katika afya ya uzazi wa mpango kutasaidia kupunguza idadi ya vijana tegemezi kwa kuwa jamii itaweza kuwa na watoto ambao wataandaliwa kwa kuwapa elimu na malezi bora.

“Kwa sasa Watanzania tegemezi ni asilimia 66.9 ambao asilimia 43.9 ni watoto wenye umri kati ya miaka 0 hadi 14, vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 ni asilimia 19.1 na umri kuanzia 65 na zaidi ni asilimia 3.9,” alisema Halima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles