MBEYA KWANZA YAIVURUGA COASTAL UNION

0
40

Na ESTHER GEORGE

TIMU ya Mbeya Kwanza imefanikiwa kuiburuza Coastal Union baada ya kuichapa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Katika mchezo huo kulikuwa na ushindani mkali, lakini mapema dakika ya nne, Chunga Saidi, aliiandikia bao la kwanza timu yake ya Mbeya Kwanza.

Dakika ya 25, Issa Nelson, aliongeza bao la pili baada ya kupiga shuti kali lililopenya moja kwa moja golini ambapo bao hilo lilidumu kipindi cha kwanza cha mchezo.

Dakika ya 78 kipindi cha pili, Raizid Yasir, alifanikiwa kuiandikia bao la kufutia machozi timu yake ya Coastal Union.

Mpaka dakika 90 za mchezo kumalizika, Mbeya Kwanza walifanikiwa kutoka kifua mbele.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha wa Mbeya Kwanza, Maka Mwalwisi, alisema licha ya kupata ushindi mchezo ulikuwa mgumu kwani wapinzani wao waliwakamia kupita kiasi lakini wakafanikiwa kupata pointi tatu ambazo anaamini zitawaweka nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here