33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa kumchanja viwembe mwanamke sehemu za siri

Erick Mugisha, Dar es salaam

Mwanamume mmoja mkazi wa Tandale kwa Mtogole jijini Dar es Salaam, Siasa Samwel (30), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kumjeruhi kwa kumkata kwa viwembe sehemu za siri mwanamke mmoja, Zaina Issah.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumkata mwanamke huyo sehemu za siri Novemba 15, mwaka jana na kumsababishia kupoteza bikra yake.

Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Veronica Mtafya, amedai tukio hilo lilitokea eneo la Tandale Chama Wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amekana shtaka hilo ambapo mwendesha mashtaka alidai upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kusomwa kesi hiyo.

Hakimu Lihamwike amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua za utambulisho, nakala ya vitambulisho na kusaini bondi ya Sh milioni moja.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya hayo na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapokuja kusomwa tena Septemba 2, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles