23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAY APATA WAKATI MGUMU KUHUSU BREXIT

 

 

LONDON, UINGEREZA


Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Boris Johnson, ameendeleza mashambulizi yake jana dhidi ya Serikali ya Waziri Mkuu Theresa May, akitabiri ushindi kwa Umoja wa Ulaya (EU) katika mazungumzo kuhusu kujitoa kwa Uingereza katika umoja huo maarufu kama Brexit.

Tangu alipojiuzulu wadhifa wake wa uwaziri wa mambo ya nje Julai mwaka huu, Johnson amekuwa akiandika makala katika gazeti la Daily Telegraph akiikosoa Serikali ya May namna inavyoshughulika na mchakato wa kujiondoa Brexit.

Johnson ambaye alikuwa mstari wa mbele wakati wa kampeni ya kura ya maoni kuhusu Brexit na baadaye kushika wadhifa wa uwaziri wa mambo ya nje wakati Uingereza ilipoanza mazungumzo kuhusu mchakato huo, alisema anahofia matokeo yasiyoepukika kuhusu mchakato huo yatakuwa ni ushindi kwa EU.

Mpango wa May pamoja na mambo mengine ni kuiondoa Uingereza kutoka soko la pamoja baada ya hatua ya Brexit, lakini akitaka ibakie katika biashara huru kwa baadhi ya bidhaa kupitia makubaliano yanayohusu ushuru wa forodha na taratibu nyingine kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo, Jonson na kundi lake wanaupinga mpango huo wa May wakisema unaifanya Uingereza kuendelea kuwa karibu zaidi na EU hata baada ya kujiondoa kwenye umoja huo Machi mwakani.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles