30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAWAZIRI AFRIKA KUJADILI UDHIBITI FEDHA HARAMU

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

BARAZA la mawaziri kutoka Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti Utakatishaji Fedha Haramu litakutana nchini kuanzia Septemba 2 hadi 6 mwaka huu visiwani Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Fedha na Mipango ilieleza kuwa mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa makatibu wakuu utakaofanyika kuanzia Septemba 2.

“Kwa sasa Tanzania ndiyo mwenyekiti  wa umoja huo kwa kipindi cha mwaka mmoja, baada ya kupokea uenyekiti kutoka Jamhuri ya Zimbabwe iliyomaliza muda wake Agosti, 2017, ambapo Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ndiye mwenyekiti ataongoza mkutano huo.

“Katika mkutano huo, pamoja na masuala mbalimbali yatakayojadiliwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itatumia fursa hiyo  kuwasilisha Taarifa ya hatua iliyofikia katika utekelezaji wa Mpango wa “Financial Action Task Force” (FATF) ulioasisiwa mwaka 2009,” ilieleza taarifa hiyo.

 

Mpango huo ulizitaka nchi wanachama kufanya tathmini ya utekelezaji wa maazimio yaliyoainishwa kwenye FATF, katika maeneo mbalimbali ya kisheria, kisera, miongozo ya kitaasisi zikiwemo sekta za fedha na maeneo ya ushirikiano wa kimataifa.

Lengo ni kubaini jinsi nchi wanachama  zilivyojipanga katika kudhibiti suala la Utakasishaji Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi .

Mbali na hatua hiyo katika mkutano huo watajadili na kupanga mbinu na mikakati mbalimbali itakayosaidia kudhibiti utakatishaji fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, hatua ambayo italeta matokeo chanya na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kufikia maendeleo tarajiwa kwa nchi wanachama.

Tanzania ni miongoni mwa nchi waanzilishi wa umoja huo ulioasisiwa jijini Arusha  mwaka 1999. Nchi nyingine ni  Uganda, Kenya, Mauritius, Namibia, Sychelles na Swaziland ambazo zilisaini makubaliano.

Makao Makuu ya Sekretariati ya Umoja huo wenye nchi wanachama (18) ambazo ni Angola, Botswana, Ethiopia, Kenya, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini, Swaziland, Sychelles, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe  kuwa jijini  Dar es Salaam Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Kwanini hamruhusu makala zenu kuwa saved? Wasomaji wengine wangependa kuweka kumbukumbu makala na story zenu. Kuna ubaya gani ku copy and paste? Tunaomba web master aliangalie hili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles