24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mawasiliano ya kijamii yakatwa Burundi

Burundi's President Pierre NkurunzizaBUJUMBURA, BURUNDI
MAMLAKA nchini Burundi zimekata mawasiliano ya mitandao ya kijamii kupitia simu za mkononi, ambayo yamekuwa yakitumika kupanga maandamano ya kumpinga Rais Pierre Nkurunziza.
Mamia ya waandamanaji wako barabarani kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kwa siku ya nne jana wakipinga uamuzi wa Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Mawasiliano hayo ni kupitia mitandao ikiwamo ya Facebook, Whatsapp, Twitter na Tango huku kituo kikuu binafsi cha redio kikiwa kimefungwa katika harakati za Serikali kuzuia kuenea kwa ujumbe unaohamasisha maandamano.
Mitandao ya jamii imekuwa ikitumika kuratibu maandamano hayo ambayo ni makubwa zaidi nchini Burundi tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005.
African Public Rasio, maarufu kama ‘Sauti ya Wasio na Sauti’, ni moja ya vituo vitatu vya redio ambavyo matangazo yake ya moja kwa moja yamesitishwa, kwa kile Serikali ilichodai kuwa vinavuruga amani.
Nkurunziza, kiongozi wa zamani wa waasi ameonya kuwa yeyote anayetaka kusababisha matatizo kwa chama tawala atajiweka mwenyewe matatani.
Watu watatu wameuawa tangu Jumapili wakati polisi walipoutawanya umati kwa risasi za moto huku makumi kwa maelfu wakiikimbia nchi.
Chini ya Katiba ya Burundi, marais wanaweza kuchaguliwa kwa mihula miwili , lakini washirika wa Nkurunziza wanasema muhula wake wa kwanza hauhesabiki kwa vile aliteuliwa na Bunge.
Nkurunziza yu madarakani tangu mwaka 2005, wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 12 vilipomalizika rasmi.
Watu zaidi ya 300,000 waliuawa katika mgogoro huo baina ya jeshi lililodhibitiwa na Watutsi walio wachache na makundi ya waasi wa Kihutu kama vile CNDD-FDD la Nkurunziza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles