24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakili wavutana mahakamani rufaa pingamizi la Mbowe, Matiko

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Upande wa utetezi kesi ya rufaa ya pingamizi la kufutiwa dhamana iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demorasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, umedai hakuna mahali walipoeleza kifungu cha sheria wakati wakitoa notisi ya kukata rufaa.

Wakili wa utetezi Peter Kibatala, amedai hayo akijibu hoja za upande wa jamhuri kuwa walitakiwa kuwasilisha rufaa chini ya kifungu cha sheria namba 359 na 361 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai.

Kibatala amedai kwamba suala la mwenendo wa kesi kuwa haujachapwa lilishatolewa uamuzi jana na Jaji Rumanyika na wakakubali ziletwe kama zilivyo.

Alidai mahakama ilitoa haki ya kusikiliza pande zote mbili katika suala la mwenendo wa kesi.

Kibatala alisema rufaa yao ina msingi hivyo aliomba isikilizwe ili washtakiwa wapate haki yao ya kikatiba ya kuwa nje kwa dhamana.

Hata hivyo, Jaji Sam Rumanyika baada ya kusikiliza hoja zote aliahirisha kesi hadi kesho kwa ajili ya kutoa uamuzi wa pingamizi la Jamhuri la kutaka rufaa itupwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles