27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakili watakiwa kuharakisha upelelezi kesi ya kina Kitilya

img_1299

Na MANENO SELANYIKA –DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewataka mawakili wa Serikali kuharakisha upelelezi wa kesi inayomkabili Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitlya na wenzake.

Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Syprian Mkeha, upande wa Serikali ulikuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Mutalemwa Kishenyi, wakati utetezi ukisimamiwa na Alex Mgongolwa.

Kishenyi alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo aliomba mahakama iahirishe shauri hilo.

“Mheshimiwa leo (jana) kesi hii imekuja kwa ajili ya kutajwa pia tumepokea maombi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwa iahirishwe kwa kuwa Takukuru nao hawajakamilisha upelelezi wao,” alisema Kishenyi.

Upande wa utetezi ulilalamika na kudai kwamba kesi bado ipo gizani kwa sababu kila inapotajwa Serikali wanasema upelelezi haujakamilika.

“Ni takribani miezi sita sasa wateja wangu wapo mahabusu, naomba mawakili wa Serikali waharakishe suala hili,” alidai Mgongolwa.

Kutokana na hoja hiyo, mahakama ilipanga kesi hiyo itajwe tena Novemba 4, mwaka huu na washtakiwa walirejeshwa tena mahabusu.

Mbali na Kitilya, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic, Sioi Solomon ambao wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali likiwemo la utakatishaji wa fedha.

Mashtaka mengine ni kutumia nyaraka za kughushi na za uongo na kujipatia isivyo halali Dola milioni sita za Marekani sawa na Sh bilioni 12, pia katika tarehe tofauti kati ya Agosti, 2012 na Machi, 2013 jijini Dar es Salaam washtakiwa walipanga kwa ushirikiano na watu wengine kujipatia fedha kutoka serikalini kwa njia ya udanganyifu.

Pia ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kati ya Agosti 2, 2012 katika Ofisi za Makao Makuu ya Stanbic Tanzania Limited zilizopo Kinondoni, Shose akiwa na nia ovu alighushi taarifa za maombi ya fedha katika Benki ya Standard.

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mbele ya mahakama hiyo Aprili, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles