27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakala wapigana vikumbo kwa Okwi

Na MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

MAWAKALA mbalimbali wameanza kupigana vikumbo katika hoteli iliyoweka kambi timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ nchini Misri inakofanyika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon2019), lengo likiwa ni kuona uwezekano wa kunasa wachezaji, akiwamo mshambuliaji hatari wa timu hiyo, Emmanuel Okwi.

Okwi amekuwa moto wa kuotea mbali katika michuano hiyo, baada ya juzi kuisadia Uganda kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya 16 bora, kutokana na sare bao 1-1 dhidi ya Zimbabwe.

Okwi aliifungia Uganda bao pekee lililoipa pointi moja katika mchezo wa pili wa michuano hiyo dhidi ya Zimbabwe, kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.

Bao hilo liliisaidia Uganda kufikisha pointi nne na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi A, linaloongozwa na wenyeji, Misri wenye pointi sita, huku Zimbabwe ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja, wakati DRC ikiburuza mkia kwa kuambulia patupu.

Bao la juzi limemwezesha Okwi kufikisha mabao mawili katika michuano hiyo, bao lake la kwanza akilifunga kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya DR Congo.

Okwi amekuwa katika kiwango cha juu katika michuano hiyo, jambo linalotia hofu kuhusu hatima yake ya kuendelea kukipiga Simba msimu ujao, hasa kutokana na jinsi mawakala kutoka klabu mbalimbali Afrika na Ulaya kumpigia hesabu.

Ikumbukwe kwa sasa Okwi ni mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili Simba, huku akiwahenyesha viongozi wa klabu hiyo katika mazungumzo ya mkataba mpya.

Habari kutoka ndani ya kambi ya The Cranes, zinasema kuwa mbali ya Okwi, mchezaji mwingine wa timu hiyo anayewafanya mawakala mbalimbali kuvamia katika hoteli waliyopo ya Radisson Blu iliyopo jijini Cairo, ni mshambuliaji wa KCCA, Patrick Kaddu aliyefunga bao dhidi ya Zimbabwe.

Mtandao wa Kawowo Sports wa Uganda, umeripoti jana ukisema: “Kiwango cha Kaddu na Okwi, kimewavuta mawakala wengi ambao wamekuwa wakiivamia hoteli iliyopo The Cranes ili kuona kama wanaweza kuwashawishi wawili hao na wengineo waliocheza vizuri dhidi ya DRC.”

Katika kuonyesha hofu ya kumpoteza Okwi, tayari Simba imeanza kujipanga upya kwa kumnasa mshambulaji raia wa Bzaril, Wilker Henrique da Silva kutoka klabu ya Bragantino inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles