31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MAVUNDE: WATANZANIA ZINGATIENI TAARIFA ZA HALI YA HEWA

|Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amewataka Watanzania kuzingatia taarifa za hali ya hewa na kuzipa uzito ili kuepukana na athari mbalimbali za mabadiliko ya tabia nchi.

Mavunde ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Taifa wa Taarifa za Huduma ya Hali ya Hewa.

“Taarifa za hali ya hewa ni muhimu kwa ustawi wa uchumi na maendeleo ya nchi kiujumla hivyo ni muhimu kupewa uzito katika mipango ya nchi na hasa katika kuelekea nchi ya uchumi wa viwanda,” amesema.

Naye Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Profesa Petteri Taalas ameipongeza Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi za Afrika zinavyofanya vizuri katika masuala ya hali ya hewa na kuahidi kuendelea kuipa ushirikiano Tanzania katika utekelezaji wa programu mbalimbali za masuala ya hali ya hewa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora amesema Idara ya Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), zitaendelea kufanya kazi kwa ukaribu ili kuhakikisha Watanzania wanaelimishwe juu ya umuhimu wa taarifa za hali ya hewa na pia kujikinga na maafa mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles