23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAUZO YA HISA YASHUKA KWA ASILIMIA 84

JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM

MAUZO ya hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) wiki hii yameshuka kwa asilimia 84 kutoka Sh trilioni 2.5 hadi Sh milioni 406, huku idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ikipungua kutoka hisa 868,000 hadi 262,000.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa DSE, Patrick Mususa, alisema hali hiyo ilichangiwa na kupungua kwa hisa zilizoingia sokoni na kusababisha mahitaji kuwa makubwa, jambo lililosababisha bei ya hisa kwa kampuni kuongezeka.

Alisema licha ya mauzo kushuka kwa kiwango hicho, ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko uliongezeka kwa Sh bilioni 300 kutoka Sh trilioni 18.7 hadi Sh trilioni 19.0, ikichangiwa na kuongezeka kwa bei ya hisa za baadhi ya kampuni.

“Mtaji wa kampuni za ndani umeendelea kubaki kwenye kiwango cha awali cha Sh trilioni 7.1 wiki iliyopita. Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa zake ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa asilimia 63.8 ikifuatiwa na Benki ya CRDB kwa asilimia 12.4 na Kampuni ya Sigara TCC kwa asilimia 8.9,” alisema Mususa.

Kuhusu viashiria vya soko, Mususa alisema kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kiliongezeka kwa pointi 35 kutoka pointi 2,146 hadi 2,181 kutokana na ongezeko la bei ya hisa za DSE, ACACIA na NMG.

“Kiashiria cha kampuni za ndani (TSI) kimeongezeka kwa pointi 0.6 kutoka 3,380.2 hadi 3.380.8 kutokana na ongezeko kwa bei ya hisa za DSE, pia sekta ya viwanda imebaki kwenye kiwango kile kile cha pointi 4.194,” alisema Mususa.

Aidha, alisema sekta ya huduma za kibenki iliongezeka kwa pointi 1.5 baada ya hisa za DSE kupanda bei kwa asilimia 6 kutoka 1,000 hadi 1,060 kwa kila hisa, huku sekta ya huduma za kibiashara nayo ikibaki kwenye kiwango cha awali cha pointi 3.137.

Wakati hali ikiwa hivyo, kampuni zote kubwa za  mawasiliano nchini tayari zimepeleka maombi katika soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ili kukidhi matakwa ya sheria yanayozitaka kufanya hivyo.

Katika Bunge la bajeti 2016/2017, Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Serikali alitahadhalisha Serikali kuhusu mapendekezo ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk Philip Mpango kwa kupendekeza kampuni za simu kulazimishwa kujiorodheshwa na kubadilishwa kwenda kwenye  soko la hisa la Dar es Salaam kwa nguvu.

Mbunge huyo alijenga hoja kwamba  pendekezo hilo lililozitaka kampuni hizo kujisahiji kabla ya miezi sita lilikuwa na upungufu mkubwa.

“Leo hii tukilazimisha kampuni zote zijioorodheshwe DES  haiwezi kuhimili na haina uwezo huo na hakuna utaratibu wa kuzuia watu wa nje kununua hisa kwa sababu sheria ya soko haizuii  mtu wa nje ya Tanzania kununua hizi hisa.

 “Listing ya kampuni iwe asilimia 35 tofauti na asilimia 25 ya Serikali na hii ni kutokana na sheria ya uwekezaji ambayo inataka asilimia 35 zimilikiwe na wananchi kupitiaa soko la hisa lakini utolewe muda kwa sababu DSE kwa kipindi cha miaka 20 free frot ya Dse ni Sh trilioni 3.7.alisema Bashe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles